Sanaa ni uzuri unao jitokeza katika umbo lililo sanifishwa Umbo ambalo Mtu hulitumia kueleza hisia zinazo mgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum.
Iyo ni moja ya maana ya sanaa kati ya zile nyingi zilizo tolewa na wana sanaa mbali mbali
Vile vile sanaa imegawanyika katika Makundi (aina) Mbali mbali ngoja tuzijadiri aina izo kwa ufupi
AINA ZA SANAA
Kuna aina kuu tatu za sanaa
(a) SANAA ZA UONYESHO
Sanaa hizi Uzuri wake Ujitokeza katika umbo LA kudumu umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuoneshwa wakati wote
Mfano wa sanaa za uonyesho ni
-Uchoraji
-Uchongaji
-Ufinyanzi
-kutarizi n.k.
(b)SANAA ZA GHIBU
Sanaa hizi uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linalo onekana kwa macho au kushikika Bali katika umbo linalo gusa hisia
Mfano wa sanaa za Ghibu no:-
-Ushahiri
-Upigaji
-Muziki n.k.
(C) SANAA ZA VITENDO/MAONYESHO
Uzuri wa Sanaa za aina hii umo katika umbo la vitendo na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika Jumbo hili lina lazimisha kuwepo kwa Mwana sanaa ,Mtazamaji na mahali panapo fanyikia Vitu hivi lazima vipatikane oamoja bila hivyo aina hii ya sanaa haikamiliki
Hapa ni mwanzo tu
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFuta