SANAA KAZI
Director Andrew Selano
Jumamosi, 16 Septemba 2017
Jumapili, 24 Januari 2016
Jumatatu, 17 Agosti 2015
FAHAMU YANAYO MPASA MONGOZAJI WA FILAM. (DIRECTOR) ep1
yMtunzi WA story baada Ya kuandika nakumpa mwandishi WA Script na kuandika Script,producer apewe hiyo ikiwa tayari. Baada Ya hapo yakupasa kumtafuta MONGOZAJI Mzuri kwa ajiri Ya production. Director baada YA Kuelewa script utaisoma Mara Ya Kwanza Mara YA pili na Mara ya Tatu.Mara YA nne utalazimika kusoma katikati YA Mstari YA Script hiyo Ili Kujua muda, matukio, matamshi YA mambo.
AINA YA WA ONGOZAJI
Kuna Aina Mbili Za waongozaji
(a) Democratic Director
-director Huyu anakubari kushauriwa katika uongozaji wake
(b) Dictetar director
-director Huyu hataki ushauri katika uongozaji wake
Mwongozaj baada ya kusoma script na kuchambua na kujua vizur lengo la mwandishi kwenye film hiyo analazimika kutumia usemi huu. CHELEWA KUINGIA, WAHI KUFIKA ENTER LATE, LATE EARLY, = usemi huu maana yake kuu inamtaka mwongozaji ( Director) kuziona scene ambazo mwandishi wa script ameziweka humo lakini hazina umuhimu hata kama hazikuwepo aziathir na kupoteza maana ya filam hiyo vilevile mwongozaj huyo anatakiwa kuzichambua tena scene zilizo bakia inawezekana baadhi ya scene zilizo baki anaweza kuziondoa na maana ya filam ikabaki Kama ilivyo kusudiwa.
MWIGIZAJI NA MWONGOZAJI
ACTER & DIRECTOR
Mwongozaji ( Director) anatakiwa kumwongoza mwigizaji, kitakachofanywa na mwigizaj lazima kiwe na maana katika scene husika
Hapa ndipo mwongozaji ( Director )
anatakiwa kujua kuna waigizaji wa aina mbili ili aweze kuandaa ubunifu katika kuwaongoza waigizaji pale itakapobidi.
Jumanne, 4 Agosti 2015
MBINU ZA UTUNGAJI WA TAMTHILIA
Kabra ya kuangalia mbinu za utungaji wa Tamthilia tuangalie kwanza dhima au kazi za tamthiliya
Tamthiliya ni aina ya kazi ya sanaa yenye kubwa kwa jamii zifuatazo ni dhima za tamthiliya kwa ufupi
(a) huburudisha, kazi moja wapo ya tamthiliya ni kuburudisha Mimi binafsi sina shaka na hili naamini wasanii wengi wanaweza kuifanya
(b) Huelimisha jamii kuhusu mambo mbali mbali hili ni swala la msingi jamii inapaswa kuelimishwa kwa kupitia sanaa hii ya tamthiliya vile vile hukosoa jamii kwa mfano kukosoa Tabia mbaya mbaya kama vile ulevi, wizi na rushwa
(C) Nichachu ya mabadiliko ,kwani huonyesha maisha name tabia zinazofaavkuigwa na jamii kwa mfano uaminifu uzalendo utii name uoendo
Vile vile tamthiliya
(D)Ni chanzo cha ajira kwa vijana name watu mbali mbali wanao igiza
Hizo ni baadhi ya kazi za tamthiliya
Tuangalie sasa
MBINU ZA UTUNGAJI WA TAMTHILIYA
Ili kuweza kutunga tamthiliya kuna mambo kadhaa ya kuzingatia . kama vile
(i) Chagua dhamira au jambo la kuandika kwamaana nyingine ni wazo kuhuu LA tamthiliya jambo hili ni la kwanza kabla ya kuanza kuandika
(ii) Pang a ploti au msuko wa matukio
Ploti ni mfululizo wa visa na matukio ndani ya tamthiliya hivyo unapotaka kuandaa tamthilia inakupasa kuamua utangulizi uhusu nini mgongoro uwe kati ya pande zipi kilele cha mgogoro kiwe nini na hitimisho au suluhisho la mgogoro liwe nini.
Buni wahusika watakao endana na kile unacho andika. Kumbuka kua wahusika kuna kua na wahusika WA aina mbili
-Wahusika wakuu
-wahusika WA dogo
Pia wahusika wakuu ndio wanao peleka igizo au tamthiliya mbele kutokana na vitendo ulivyo watengenezea kwa mfano kama muhusika wako anacheza kama mtu msomi basi tunategemea anatumia lugha fasaha
( iii) Chagua Madhari yanayofaa kwaajili ya wahusika na jambo unalo andika.
(iv) Tumia mtindo wa majibizano au mazungumzo kati ya wahusika mfano
Selano: sikuhizi ume badilika
Sanaa
Boyseb: nime kuwa mnene sana
au mwembaba sana?
Selano: hapana yani umebadilika
Kitabia tifauti na kipindi
tupo shule.
Boyseb: selano maisha yana
Badirika yatupasa tuishi
Kulingana na nyakati
(v)Weka maelekezo ya jukwaa. Haya uwekwa mwanzo WA onyesho au katikati ya mazungumzo ya wahusika. Maelekezo ya jukwaa uandikwa kwa italiki
Kwa mfano
Ni giza. Eneo lina miti mingi na zinasikika sauti za ndege na wadudu mbali mbali.Cheche na Tamba wamejificha nyuma ya kichaka kimojawapo
Chechen: (Akiongea kwa sauti ya
Nimrsikia kama kijiti kimevunjika. Nadhani watakuwa wamepita upande ule kule. (anaonyesha kwa kidore upande wa mbele yao).
Tamba: (Anaongelea sikioni mwa Cheche) Ndiyo ! Naona kama kuna kitu kinapita.(anaonyesha kidole) Ona pale ! Ona pale! Ah! Hao ni wenyewe kabisa.
(Vi) Tumia lugha ya kisanii kama vile tamathali za semi Methali nahau na misemo
Pia tumia ucheshi taharuki takriri na matumizi ya taswila .
Jumatatu, 3 Agosti 2015
TAMTHILIA
Tamthilia ni hadithi iliyo buniwa au kutolewa kwa lengo la kueleza Dhamira Fulani kwa njia ya vitendo na maneno mbele ya hadhira
Muigizaji wa tamthilia anatakiwa kushirikiana na hadhira moja kwa moja kwa kupitia hisia , ishara au vitendo vyake katika igizo linalo husika
AINA ZA TAMTHILIA
Kuna aina kuu nne za tamthilia
(a) TANZIA
Tanzia ni tamthilia zinazojengwa name visa vituko pamoja na migogoro na hatima yake ni kifo kwa mhusika mkuu au jamii
(b)TUFAHI
Tamthilia hizi hujengwa na visa vituko na migogoro ambayo huishia kwenye furaha na ushindi
(C) YUGA
Ni yamthilia hambazo huonyesha furaha na huzuni kwa wakati mmoja na kuwafanya watazamaji wa furahie vichekesho vilivyomo
(D)RANSA
Ni tamthilia zinazo husu utani name kusahihishana au kejeri name mzaha WA kweli
Iyo ndio tamthilia kwa ufupi
Jumapili, 2 Agosti 2015
MAANA YA SANAA
Sanaa ni uzuri unao jitokeza katika umbo lililo sanifishwa Umbo ambalo Mtu hulitumia kueleza hisia zinazo mgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum.
Iyo ni moja ya maana ya sanaa kati ya zile nyingi zilizo tolewa na wana sanaa mbali mbali
Vile vile sanaa imegawanyika katika Makundi (aina) Mbali mbali ngoja tuzijadiri aina izo kwa ufupi
AINA ZA SANAA
Kuna aina kuu tatu za sanaa
(a) SANAA ZA UONYESHO
Sanaa hizi Uzuri wake Ujitokeza katika umbo LA kudumu umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuoneshwa wakati wote
Mfano wa sanaa za uonyesho ni
-Uchoraji
-Uchongaji
-Ufinyanzi
-kutarizi n.k.
(b)SANAA ZA GHIBU
Sanaa hizi uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linalo onekana kwa macho au kushikika Bali katika umbo linalo gusa hisia
Mfano wa sanaa za Ghibu no:-
-Ushahiri
-Upigaji
-Muziki n.k.
(C) SANAA ZA VITENDO/MAONYESHO
Uzuri wa Sanaa za aina hii umo katika umbo la vitendo na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika Jumbo hili lina lazimisha kuwepo kwa Mwana sanaa ,Mtazamaji na mahali panapo fanyikia Vitu hivi lazima vipatikane oamoja bila hivyo aina hii ya sanaa haikamiliki
Hapa ni mwanzo tu